ق Qaaf
(1) Qaaf. Naapa kwa Qur'ani tukufu!
(2) Bali wanastaajabu kwamba amewafikia mwonyaji kutoka miongoni mwao, na wakasema makafiri: Hili ni jambo la ajabu!
(3) Ati tukifa na tukawa udongo...? Kurejea huko kuko mbali!
(4) Hakika Sisi tunajua kiasi cha kila kinacho punguzwa na ardhi kutokana nao. Na kwetu kipo Kitabu kinacho hifadhi yote.
(5) Lakini waliikanusha Haki ilipo wajia; kwa hivyo wamo katika mambo ya mkorogo.
(6) Je! Hawaangalii mbingu zilizo juu yao! Vipi tulivyo zijenga, na tukazipamba. Wala hazina nyufa.
(7) Na ardhi tumeitandaza na tukaiwekea milima, na tukaiotesha mimea mizuri ya kila namna.
(8) Yawe haya ni kifumbua macho na ukumbusho kwa kila mja mwenye kuelekea.
(9) Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji yaliyo barikiwa, na kwa hayo tukaotesha mabustani na nafaka za kuvunwa.
(10) Na mitende mirefu yenye makole yaliyo zaa kwa wingi,
(11) Ili iwe ni riziki kwa waja wangu. Na tukaifufua kwa maji nchi iliyo kuwa imekufa. Kama hivyo ndivyo utakavyo kuwa ufufuaji.
(12) Kabla yao walikadhibisha kaumu ya Nuhu na wakaazi wa Rassi na Thamudi.
(13) Na A'di na Firauni na kaumu ya Lut'i.
(14) Na wakaazi wa Machakani, na watu wa Tubbaa'. Wote hao waliwakanusha Mitume, kwa hivyo onyo likathibitika juu yao.
(15) Kwani tulichoka kwa kuumba mara ya kwanza. Bali wao wamo katika shaka tu juu ya umbo jipya.