الصافات   سورة  : As-Saaffaat


سورة Sura   الصافات   As-Saaffaat
الصافات As-Saaffaat
وَالصَّافَّاتِ صَفًّا (1) فَالزَّاجِرَاتِ زَجْرًا (2) فَالتَّالِيَاتِ ذِكْرًا (3) إِنَّ إِلَٰهَكُمْ لَوَاحِدٌ (4) رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَرَبُّ الْمَشَارِقِ (5) إِنَّا زَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِزِينَةٍ الْكَوَاكِبِ (6) وَحِفْظًا مِّن كُلِّ شَيْطَانٍ مَّارِدٍ (7) لَّا يَسَّمَّعُونَ إِلَى الْمَلَإِ الْأَعْلَىٰ وَيُقْذَفُونَ مِن كُلِّ جَانِبٍ (8) دُحُورًا ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ وَاصِبٌ (9) إِلَّا مَنْ خَطِفَ الْخَطْفَةَ فَأَتْبَعَهُ شِهَابٌ ثَاقِبٌ (10) فَاسْتَفْتِهِمْ أَهُمْ أَشَدُّ خَلْقًا أَم مَّنْ خَلَقْنَا ۚ إِنَّا خَلَقْنَاهُم مِّن طِينٍ لَّازِبٍ (11) بَلْ عَجِبْتَ وَيَسْخَرُونَ (12) وَإِذَا ذُكِّرُوا لَا يَذْكُرُونَ (13) وَإِذَا رَأَوْا آيَةً يَسْتَسْخِرُونَ (14) وَقَالُوا إِنْ هَٰذَا إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ (15) أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ (16) أَوَآبَاؤُنَا الْأَوَّلُونَ (17) قُلْ نَعَمْ وَأَنتُمْ دَاخِرُونَ (18) فَإِنَّمَا هِيَ زَجْرَةٌ وَاحِدَةٌ فَإِذَا هُمْ يَنظُرُونَ (19) وَقَالُوا يَا وَيْلَنَا هَٰذَا يَوْمُ الدِّينِ (20) هَٰذَا يَوْمُ الْفَصْلِ الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ (21) ۞ احْشُرُوا الَّذِينَ ظَلَمُوا وَأَزْوَاجَهُمْ وَمَا كَانُوا يَعْبُدُونَ (22) مِن دُونِ اللَّهِ فَاهْدُوهُمْ إِلَىٰ صِرَاطِ الْجَحِيمِ (23) وَقِفُوهُمْ ۖ إِنَّهُم مَّسْئُولُونَ (24)
الصفحة Page 446
الصافات As-Saaffaat
(1) Naapa kwa wanao jipanga kwa safu.
(2) Na kwa wenye kukataza mabaya.
(3) Na kwa wenye kusoma Ukumbusho.
(4) Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja.
(5) Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yao, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote.
(6) Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota.
(7) Na kulinda na kila shet'ani a'si.
(8) Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande.
(9) Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu.
(10) Isipo kuwa anaye nyakua kitu kidogo, na mara humfwatia kimondo kinacho ng'ara.
(11) Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tulio waumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unao nata.
(12) Bali unastaajabu, na wao wanafanya maskhara.
(13) Na wanapo kumbushwa hawakumbuki.
(14) Na wanapo ona Ishara, wanafanya maskhara.
(15) Na husema: Haya si chochote ila ni uchawi tu ulio dhaahiri.
(16) Ati tukisha kufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa?
(17) Hata baba zetu wa zamani?
(18) Sema: Naam! Hali nanyi ni madhalili.
(19) Huko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndio wataona!
(20) Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo.
(21) Hii ndiyo Siku ya Hukumu mliyo kuwa mkiikadhibisha.
(22) Wakusanyeni walio dhulumu, na wake zao, na hao walio kuwa wakiwaabudu -
(23) Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu!
(24) Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa:
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022