القيامة   سورة  : Al-Qiyaama


سورة Sura   القيامة   Al-Qiyaama
فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ (48) فَمَا لَهُمْ عَنِ التَّذْكِرَةِ مُعْرِضِينَ (49) كَأَنَّهُمْ حُمُرٌ مُّسْتَنفِرَةٌ (50) فَرَّتْ مِن قَسْوَرَةٍ (51) بَلْ يُرِيدُ كُلُّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُؤْتَىٰ صُحُفًا مُّنَشَّرَةً (52) كَلَّا ۖ بَل لَّا يَخَافُونَ الْآخِرَةَ (53) كَلَّا إِنَّهُ تَذْكِرَةٌ (54) فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ (55) وَمَا يَذْكُرُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّهُ ۚ هُوَ أَهْلُ التَّقْوَىٰ وَأَهْلُ الْمَغْفِرَةِ (56)
القيامة Al-Qiyaama
لَا أُقْسِمُ بِيَوْمِ الْقِيَامَةِ (1) وَلَا أُقْسِمُ بِالنَّفْسِ اللَّوَّامَةِ (2) أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَلَّن نَّجْمَعَ عِظَامَهُ (3) بَلَىٰ قَادِرِينَ عَلَىٰ أَن نُّسَوِّيَ بَنَانَهُ (4) بَلْ يُرِيدُ الْإِنسَانُ لِيَفْجُرَ أَمَامَهُ (5) يَسْأَلُ أَيَّانَ يَوْمُ الْقِيَامَةِ (6) فَإِذَا بَرِقَ الْبَصَرُ (7) وَخَسَفَ الْقَمَرُ (8) وَجُمِعَ الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ (9) يَقُولُ الْإِنسَانُ يَوْمَئِذٍ أَيْنَ الْمَفَرُّ (10) كَلَّا لَا وَزَرَ (11) إِلَىٰ رَبِّكَ يَوْمَئِذٍ الْمُسْتَقَرُّ (12) يُنَبَّأُ الْإِنسَانُ يَوْمَئِذٍ بِمَا قَدَّمَ وَأَخَّرَ (13) بَلِ الْإِنسَانُ عَلَىٰ نَفْسِهِ بَصِيرَةٌ (14) وَلَوْ أَلْقَىٰ مَعَاذِيرَهُ (15) لَا تُحَرِّكْ بِهِ لِسَانَكَ لِتَعْجَلَ بِهِ (16) إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُ وَقُرْآنَهُ (17) فَإِذَا قَرَأْنَاهُ فَاتَّبِعْ قُرْآنَهُ (18) ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ (19)
الصفحة Page 577
(48) Basi hautawafaa kitu uombezi wa waombezi.
(49) Basi wana nini hata wanapuuza onyo hili?
(50) Kama kwamba wao ni mapunda walio timuliwa,
(51) Wanao mkimbia simba!
(52) Ati kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizo funuliwa.
(53) Hasha! Kwani wao hawaiogopi Akhera?
(54) Hasha! Kwa hakika huu ni ukumbusho!
(55) Basi anaye taka atakumbuka.
(56) Na hawatakumbuka isipo kuwa Mwenyezi Mungu atake. Uchamngu ni kwake Yeye, na msamaha ni wake Yeye.
القيامة Al-Qiyaama
(1) Ninaapa kwa Siku ya Kiyama!
(2) Na ninaapa kwa nafsi inayo jilaumu!
(3) Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake?
(4) Kwani! Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!
(5) Lakini mtu anataka tu kuendelea na maasi kwa siku zilioko mbele yake.
(6) Anauliza: Lini itakuwa hiyo Siku ya Kiyama?
(7) Basi jicho litapo dawaa,
(8) Na mwezi utapo patwa,
(9) Na likakusanywa jua na mwezi,
(10) Siku hiyo mtu atasema: Yako wapi makimbilio?
(11) La! Hapana pa kukimbilia!
(12) Siku hiyo pa kutua ni kwa Mola wako Mlezi tu.
(13) Siku hiyo ataambiwa aliyo yatanguliza na aliyo yaakhirisha.
(14) Bali mtu ni hoja juu ya nafsi yake.
(15) Na ingawa atatoa chungu ya udhuru.
(16) Usiutikisie huu wahyi ulimi wako kwa kuufanyia haraka.
(17) Hakika ni juu yetu kuukusanya na kuusomesha.
(18) Tunapo usoma, basi nawe fuatiliza kusoma kwake.
(19) Kisha ni juu yetu kuubainisha.
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022