(20) Hasha! Bali nyinyi mnapenda maisha ya duniani,
(21) Na mnaacha maisha ya Akhera.
(22) Zipo nyuso siku hiyo zitao ng'ara,
(23) Zinamwangallia Mola wao Mlezi.
(24) Na zipo nyuso siku hiyo zitakao kunjana.
(25) Zitajua ya kuwa zitafikiwa na livunjalo uti wa mgongo.
(26) La, hasha! (Roho) itakapo fikia kwenye mafupa ya koo,
(27) Na pakasemwa: Nani wa kumganga?
(28) Na mwenyewe akajua kwa hakika kuwa huko ndiko kufariki;
(29) Na utapo ambatishwa muundi kwa muundi,
(30) Siku hiyo ndiyo kuchungwa kupelekwa kwa Mola wako Mlezi!
(31) Kwa sababu hakusadiki, wala hakusali.
(32) Bali alikanusha, na akageuka.
(33) Kisha akenda kwa ahali zake kwa matao.
(34) Ole wako, ole wako!
(35) Kisha Ole wako, ole wako!
(36) Ati anadhani binaadamu kuwa ataachwa bure?
(37) Kwani hakuwa yeye tone ya manii lilio shushwa?
(38) Kisha akawa kidonge cha damu, tena Mwenyezi Mungu akamuumba na akamtengeneza vilivyo.
(39) Kisha akamfanya namna mbili, mwanamume na mwanamke.
(40) Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu?
الانسان Al-Insaan
(1) Hakika kilimpitia binaadamu kipindi katika zama ambacho kwamba hakuwa kitu kinacho tajwa.
(2) Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo changanyika, tumfanyie mtihani. Kwa hivyo tukamfanya mwenye kusikia, mwenye kuona.
(3) Hakika Sisi tumembainishia Njia. Ama ni mwenye kushukuru, au mwenye kukufuru.
(4) Hakika Sisi tumewaandalia makafiri minyororo na pingu na Moto mkali.
(5) Hakika watu wema watakunywa katika vinywaji vilivyo changanyika na kafuri,