الحجر   سورة  : Al-Hijr


سورة Sura   الحجر   Al-Hijr
الحجر Al-Hijr
الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ وَقُرْآنٍ مُّبِينٍ (1) رُّبَمَا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْ كَانُوا مُسْلِمِينَ (2) ذَرْهُمْ يَأْكُلُوا وَيَتَمَتَّعُوا وَيُلْهِهِمُ الْأَمَلُ ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ (3) وَمَا أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ إِلَّا وَلَهَا كِتَابٌ مَّعْلُومٌ (4) مَّا تَسْبِقُ مِنْ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسْتَأْخِرُونَ (5) وَقَالُوا يَا أَيُّهَا الَّذِي نُزِّلَ عَلَيْهِ الذِّكْرُ إِنَّكَ لَمَجْنُونٌ (6) لَّوْ مَا تَأْتِينَا بِالْمَلَائِكَةِ إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ (7) مَا نُنَزِّلُ الْمَلَائِكَةَ إِلَّا بِالْحَقِّ وَمَا كَانُوا إِذًا مُّنظَرِينَ (8) إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ (9) وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِي شِيَعِ الْأَوَّلِينَ (10) وَمَا يَأْتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ (11) كَذَٰلِكَ نَسْلُكُهُ فِي قُلُوبِ الْمُجْرِمِينَ (12) لَا يُؤْمِنُونَ بِهِ ۖ وَقَدْ خَلَتْ سُنَّةُ الْأَوَّلِينَ (13) وَلَوْ فَتَحْنَا عَلَيْهِم بَابًا مِّنَ السَّمَاءِ فَظَلُّوا فِيهِ يَعْرُجُونَ (14) لَقَالُوا إِنَّمَا سُكِّرَتْ أَبْصَارُنَا بَلْ نَحْنُ قَوْمٌ مَّسْحُورُونَ (15)
الصفحة Page 262
الحجر Al-Hijr
(1) Alif Lam Ra. (A. L. R). Hizi ni Aya za Kitabu na Qur'ani inayo bainisha.
(2) HUENDA ikawa walio kufuru wakatamani wange kuwa Waislamu.
(3) Waache wale, na wastarehe, na iwazuge tamaa. Watakuja jua.
(4) Na hatukuuangamiza mji wowote ule ila ulikuwa na muda wake maalumu.
(5) Hawawezi watu wowote kuitangulia ajali yao, wala kuchelewa.
(6) Na walisema: Ewe uliyeteremshiwa Ukumbusho! Hakika wewe ni mwendawazimu.
(7) Mbona hutuletei Malaika ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli?
(8) Sisi hatuwateremshi Malaika ila kwa sababu ya haki, na hapo hawatapewa muhula.
(9) Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda.
(10) Na hakika tulikwisha watumia Mitume mataifa ya mwanzo.
(11) Na hakuwafikia Mtume ila walimkejeli.
(12) Na kama hivi ndivyo tunavyo ingiza katika nyoyo za wakosefu.
(13) Hawayaamini haya, na hali ya kuwa umekwisha wapitia mfano wa watu wa kale.
(14) Na lau tungeli wafungulia mlango wa mbingu, wakawa wanapanda,
(15) Basi wangeli sema: Macho yetu yamelevywa, bali sisi wenyewe tumerogwa.
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022