المطففين   سورة  : Al-Mutaffifin


سورة Sura   المطففين   Al-Mutaffifin
كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٍ (7) وَمَا أَدْرَاكَ مَا سِجِّينٌ (8) كِتَابٌ مَّرْقُومٌ (9) وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ (10) الَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ (11) وَمَا يُكَذِّبُ بِهِ إِلَّا كُلُّ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ (12) إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ (13) كَلَّا ۖ بَلْ ۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ (14) كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ (15) ثُمَّ إِنَّهُمْ لَصَالُو الْجَحِيمِ (16) ثُمَّ يُقَالُ هَٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ (17) كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْأَبْرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ (18) وَمَا أَدْرَاكَ مَا عِلِّيُّونَ (19) كِتَابٌ مَّرْقُومٌ (20) يَشْهَدُهُ الْمُقَرَّبُونَ (21) إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ (22) عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ (23) تَعْرِفُ فِي وُجُوهِهِمْ نَضْرَةَ النَّعِيمِ (24) يُسْقَوْنَ مِن رَّحِيقٍ مَّخْتُومٍ (25) خِتَامُهُ مِسْكٌ ۚ وَفِي ذَٰلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ الْمُتَنَافِسُونَ (26) وَمِزَاجُهُ مِن تَسْنِيمٍ (27) عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا الْمُقَرَّبُونَ (28) إِنَّ الَّذِينَ أَجْرَمُوا كَانُوا مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا يَضْحَكُونَ (29) وَإِذَا مَرُّوا بِهِمْ يَتَغَامَزُونَ (30) وَإِذَا انقَلَبُوا إِلَىٰ أَهْلِهِمُ انقَلَبُوا فَكِهِينَ (31) وَإِذَا رَأَوْهُمْ قَالُوا إِنَّ هَٰؤُلَاءِ لَضَالُّونَ (32) وَمَا أُرْسِلُوا عَلَيْهِمْ حَافِظِينَ (33) فَالْيَوْمَ الَّذِينَ آمَنُوا مِنَ الْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ (34)
الصفحة Page 588
(7) Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin.
(8) Unajua nini Sijjin?
(9) Kitabu kilicho andikwa.
(10) Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha!
(11) Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo.
(12) Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi.
(13) Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale!
(14) Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma.
(15) Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi.
(16) Kisha wataingia Motoni!
(17) Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha.
(18) Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I'liyyin.
(19) Na nini kitakacho kujuvya nini I'liyyin?
(20) Kitabu kilicho andikwa.
(21) Wanakishuhudia walio karibishwa.
(22) Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema.
(23) Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia.
(24) Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema,
(25) Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri,
(26) Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana.
(27) Na mchanganyiko wake ni Tasniim,
(28) Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa.
(29) Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini.
(30) Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana.
(31) Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi.
(32) Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea.
(33) Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao.
(34) Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri,
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022