الفجر   سورة  : Al-Fajr


سورة Sura   الفجر   Al-Fajr
الفجر Al-Fajr
وَالْفَجْرِ (1) وَلَيَالٍ عَشْرٍ (2) وَالشَّفْعِ وَالْوَتْرِ (3) وَاللَّيْلِ إِذَا يَسْرِ (4) هَلْ فِي ذَٰلِكَ قَسَمٌ لِّذِي حِجْرٍ (5) أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ (6) إِرَمَ ذَاتِ الْعِمَادِ (7) الَّتِي لَمْ يُخْلَقْ مِثْلُهَا فِي الْبِلَادِ (8) وَثَمُودَ الَّذِينَ جَابُوا الصَّخْرَ بِالْوَادِ (9) وَفِرْعَوْنَ ذِي الْأَوْتَادِ (10) الَّذِينَ طَغَوْا فِي الْبِلَادِ (11) فَأَكْثَرُوا فِيهَا الْفَسَادَ (12) فَصَبَّ عَلَيْهِمْ رَبُّكَ سَوْطَ عَذَابٍ (13) إِنَّ رَبَّكَ لَبِالْمِرْصَادِ (14) فَأَمَّا الْإِنسَانُ إِذَا مَا ابْتَلَاهُ رَبُّهُ فَأَكْرَمَهُ وَنَعَّمَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَكْرَمَنِ (15) وَأَمَّا إِذَا مَا ابْتَلَاهُ فَقَدَرَ عَلَيْهِ رِزْقَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَهَانَنِ (16) كَلَّا ۖ بَل لَّا تُكْرِمُونَ الْيَتِيمَ (17) وَلَا تَحَاضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ (18) وَتَأْكُلُونَ التُّرَاثَ أَكْلًا لَّمًّا (19) وَتُحِبُّونَ الْمَالَ حُبًّا جَمًّا (20) كَلَّا إِذَا دُكَّتِ الْأَرْضُ دَكًّا دَكًّا (21) وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا (22) وَجِيءَ يَوْمَئِذٍ بِجَهَنَّمَ ۚ يَوْمَئِذٍ يَتَذَكَّرُ الْإِنسَانُ وَأَنَّىٰ لَهُ الذِّكْرَىٰ (23)
الصفحة Page 593
الفجر Al-Fajr
(1) Naapa kwa alfajiri,
(2) Na kwa masiku kumi,
(3) Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja,
(4) Na kwa usiku unapo pita,
(5) Je! Hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili?
(6) Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo wafanya kina A'di?
(7) Wa Iram, wenye majumba marefu?
(8) Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi?
(9) Na Thamudi walio chonga majabali huko bondeni?
(10) Na Firauni mwenye vigingi?
(11) Ambao walifanya jeuri katika nchi?
(12) Wakakithirisha humo ufisadi?
(13) Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu.
(14) Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia.
(15) Ama mtu anapo jaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu!
(16) Na ama anapo mjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge!
(17) Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima,
(18) Wala hamhimizani kulisha masikini;
(19) Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa,
(20) Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi.
(21) Sivyo hivyo! Itakapo vunjwa ardhi vipande vipande,
(22) Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu,
(23) Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini?
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022