المسد   سورة  : Al-Masad


سورة Sura   المسد   Al-Masad
الصفحة Page 603
الكافرون Al-Kaafiroon
(1) Sema: Enyi makafiri!
(2) Siabudu mnacho kiabudu;
(3) Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.
(4) Wala sitaabudu mnacho abudu.
(5) Wala nyinyi hamuabudu ninaye muabudu.
(6) Nyinyi mna dini yenu, nami nina Dini yangu.
النصر An-Nasr
(1) Itakapo kuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi,
(2) Na ukaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi,
(3) Zitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umwombe msamaha; hakika Yeye ndiye anaye pokea toba.
المسد Al-Masad
(1) Imeangamia mikono ya Abu Lahab, na yeye pia ameangamia.
(2) Hayatamfaa mali yake, wala alivyo vichuma.
(3) Atauingia Moto wenye mwako.
(4) Na mkewe, mchukuzi wa kuni,
(5) Shingoni mwake iko kamba iliyo sokotwa.
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022