القارعة   سورة  : Al-Qaari'a


سورة Sura   القارعة   Al-Qaari'a
الصفحة Page 600
(10) Na yakakusanywa yaliomo vifuani?
(11) Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote!
القارعة Al-Qaari'a
(1) Inayo gonga!
(2) Nini Inayo gonga?
(3) Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga?
(4) Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika;
(5) Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa!
(6) Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito,
(7) Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza.
(8) Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu,
(9) Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya!
(10) Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo?
(11) Ni Moto mkali!
التكاثر At-Takaathur
(1) Kumekushughulisheni kutafuta wingi,
(2) Mpaka mje makaburini!
(3) Sivyo hivyo! Mtakuja jua!
(4) Tena sivyo hivyo! Mtakuja jua!
(5) Sivyo hivyo! Lau mngeli jua kwa ujuzi wa yakini,
(6) Basi bila ya shaka mtaiona Jahannamu!
(7) Tena, bila ya shaka, mtaiona kwa jicho la yakini.
(8) Tena bila ya shaka mtaulizwa siku hiyo juu ya neema.
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022