النبإ   سورة  : An-Naba


سورة Sura   النبإ   An-Naba
النبإ An-Naba
عَمَّ يَتَسَاءَلُونَ (1) عَنِ النَّبَإِ الْعَظِيمِ (2) الَّذِي هُمْ فِيهِ مُخْتَلِفُونَ (3) كَلَّا سَيَعْلَمُونَ (4) ثُمَّ كَلَّا سَيَعْلَمُونَ (5) أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ مِهَادًا (6) وَالْجِبَالَ أَوْتَادًا (7) وَخَلَقْنَاكُمْ أَزْوَاجًا (8) وَجَعَلْنَا نَوْمَكُمْ سُبَاتًا (9) وَجَعَلْنَا اللَّيْلَ لِبَاسًا (10) وَجَعَلْنَا النَّهَارَ مَعَاشًا (11) وَبَنَيْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعًا شِدَادًا (12) وَجَعَلْنَا سِرَاجًا وَهَّاجًا (13) وَأَنزَلْنَا مِنَ الْمُعْصِرَاتِ مَاءً ثَجَّاجًا (14) لِّنُخْرِجَ بِهِ حَبًّا وَنَبَاتًا (15) وَجَنَّاتٍ أَلْفَافًا (16) إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ كَانَ مِيقَاتًا (17) يَوْمَ يُنفَخُ فِي الصُّورِ فَتَأْتُونَ أَفْوَاجًا (18) وَفُتِحَتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ أَبْوَابًا (19) وَسُيِّرَتِ الْجِبَالُ فَكَانَتْ سَرَابًا (20) إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتْ مِرْصَادًا (21) لِّلطَّاغِينَ مَآبًا (22) لَّابِثِينَ فِيهَا أَحْقَابًا (23) لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرْدًا وَلَا شَرَابًا (24) إِلَّا حَمِيمًا وَغَسَّاقًا (25) جَزَاءً وِفَاقًا (26) إِنَّهُمْ كَانُوا لَا يَرْجُونَ حِسَابًا (27) وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا كِذَّابًا (28) وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ كِتَابًا (29) فَذُوقُوا فَلَن نَّزِيدَكُمْ إِلَّا عَذَابًا (30)
الصفحة Page 582
النبإ An-Naba
(1) WANAULIZANA nini?
(2) Ile khabari kuu,
(3) Ambayo kwayo wanakhitalifiana.
(4) La! Karibu watakuja jua.
(5) Tena la! Karibu watakuja jua.
(6) Kwani hatukuifanya ardhi kama tandiko?
(7) Na milima kama vigingi?
(8) Na tukakuumbeni kwa jozi?
(9) Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko?
(10) Na tukaufanya usiku ni nguo?
(11) Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha?
(12) Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu?
(13) Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto;
(14) Na tukateremsha maji yanayo anguka kwa kasi kutoka mawinguni,
(15) Ili tutoe kwayo nafaka na mimea,
(16) Na mabustani yenye miti iliyo kamatana.
(17) Hakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake,
(18) Siku litapo pulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa makundi,
(19) Na mbingu zitafunguliwa, ziwe milango,
(20) Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi.
(21) Hakika Jahannamu inangojea!
(22) Kwa walio asi ndio makaazi yao,
(23) Wakae humo karne baada ya karne,
(24) Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji,
(25) Ila maji yamoto sana na usaha,
(26) Ndio jaza muwafaka.
(27) Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hisabu.
(28) Na wakikanusha Aya zetu kwa nguvu.
(29) Na kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika.
(30) Basi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu!
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022