قريش Quraish
(1) Kwa walivyo zoea Maqureshi,
(2) Kuzoea kwao safari za siku za baridi na siku za joto.
(3) Basi nawamuabudu Mola Mlezi wa Nyumba hii,
(4) Ambaye anawalisha wasipate njaa, na anawalinda na khofu.
الماعون Al-Maa'un
(1) Je! Umemwona anaye kadhibisha Malipo?
(2) Huyo ndiye anaye msukuma yatima,
(3) Wala hahimizi kumlisha masikini.
(4) Basi, ole wao wanao sali,
(5) Ambao wanapuuza Sala zao;
(6) Ambao wanajionyesha,
(7) Nao huku wanazuia msaada.
الكوثر Al-Kawthar
(1) Hakika tumekupa kheri nyingi.
(2) Basi sali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi.
(3) Hakika anaye kuchukia ndiye aliye mpungufu.