الحجر   سورة  : Al-Hijr


سورة Sura   الحجر   Al-Hijr
إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا قَالَ إِنَّا مِنكُمْ وَجِلُونَ (52) قَالُوا لَا تَوْجَلْ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ (53) قَالَ أَبَشَّرْتُمُونِي عَلَىٰ أَن مَّسَّنِيَ الْكِبَرُ فَبِمَ تُبَشِّرُونَ (54) قَالُوا بَشَّرْنَاكَ بِالْحَقِّ فَلَا تَكُن مِّنَ الْقَانِطِينَ (55) قَالَ وَمَن يَقْنَطُ مِن رَّحْمَةِ رَبِّهِ إِلَّا الضَّالُّونَ (56) قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا الْمُرْسَلُونَ (57) قَالُوا إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ (58) إِلَّا آلَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمْ أَجْمَعِينَ (59) إِلَّا امْرَأَتَهُ قَدَّرْنَا ۙ إِنَّهَا لَمِنَ الْغَابِرِينَ (60) فَلَمَّا جَاءَ آلَ لُوطٍ الْمُرْسَلُونَ (61) قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ (62) قَالُوا بَلْ جِئْنَاكَ بِمَا كَانُوا فِيهِ يَمْتَرُونَ (63) وَأَتَيْنَاكَ بِالْحَقِّ وَإِنَّا لَصَادِقُونَ (64) فَأَسْرِ بِأَهْلِكَ بِقِطْعٍ مِّنَ اللَّيْلِ وَاتَّبِعْ أَدْبَارَهُمْ وَلَا يَلْتَفِتْ مِنكُمْ أَحَدٌ وَامْضُوا حَيْثُ تُؤْمَرُونَ (65) وَقَضَيْنَا إِلَيْهِ ذَٰلِكَ الْأَمْرَ أَنَّ دَابِرَ هَٰؤُلَاءِ مَقْطُوعٌ مُّصْبِحِينَ (66) وَجَاءَ أَهْلُ الْمَدِينَةِ يَسْتَبْشِرُونَ (67) قَالَ إِنَّ هَٰؤُلَاءِ ضَيْفِي فَلَا تَفْضَحُونِ (68) وَاتَّقُوا اللَّهَ وَلَا تُخْزُونِ (69) قَالُوا أَوَلَمْ نَنْهَكَ عَنِ الْعَالَمِينَ (70)
الصفحة Page 265
(52) Walipo ingia kwake na wakasema: Salama! Yeye akasema: Hakika sisi tunakuogopeni.
(53) Wakasema: Usiogope. Sisi tunakubashiria kijana mwenye ujuzi.
(54) Akasema: Mnanibashiria nami uzee umenishika! Basi kwa njia gani mnanibashiria?
(55) Wakasema: Tunakubashiria kwa haki; basi usiwe miongoni mwa wanao kata tamaa.
(56) Akasema: Na nani anaye kata tamaa na rehema ya Mola wake Mlezi ila wale walio potea?
(57) Akasema: Hebu nini amri yenu, enyi wajumbe?
(58) Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya wakosefu!
(59) Isipo kuwa walio mfuata Luut'i. Bila ya shaka sisi tutawaokoa hao wote.
(60) Ila mkewe. Tunakadiria huyo atakuwa miongoni watao bakia nyuma.
(61) Basi wale wajumbe walipo fika kwa Luut'i,
(62) Alisema (Luut'i): Hakika nyinyi ni watu msio juulikana.
(63) Wakasema: Bali sisi tumekuletea yale waliyo kuwa wakiyafanyia shaka.
(64) Na tumefika kwako kwa Haki, na hakika sisi tunasema kweli.
(65) Basi ondoka na ahli zako usiku ungalipo, nawe ufuate nyuma yao, wala yeyote kati yenu asigeuke nyuma. Na mwende mnapo amrishwa.
(66) Na tukamfunulia hukumu hiyo, ya kwamba hata wa mwisho wao hao ikifika asubuhi atakuwa kesha katiliwa mbali.
(67) Na wakaja watu wa mji ule nao furahani.
(68) Akasema: Hakika hawa wageni wangu, basi msinifedheheshe.
(69) Na mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi.
(70) Wakasema: Sisi hatukukukataza usimkaribishe yeyote?
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022