المرسلات   سورة  : Al-Mursalaat


سورة Sura   المرسلات   Al-Mursalaat
أَلَمْ نَخْلُقكُّم مِّن مَّاءٍ مَّهِينٍ (20) فَجَعَلْنَاهُ فِي قَرَارٍ مَّكِينٍ (21) إِلَىٰ قَدَرٍ مَّعْلُومٍ (22) فَقَدَرْنَا فَنِعْمَ الْقَادِرُونَ (23) وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ (24) أَلَمْ نَجْعَلِ الْأَرْضَ كِفَاتًا (25) أَحْيَاءً وَأَمْوَاتًا (26) وَجَعَلْنَا فِيهَا رَوَاسِيَ شَامِخَاتٍ وَأَسْقَيْنَاكُم مَّاءً فُرَاتًا (27) وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ (28) انطَلِقُوا إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ (29) انطَلِقُوا إِلَىٰ ظِلٍّ ذِي ثَلَاثِ شُعَبٍ (30) لَّا ظَلِيلٍ وَلَا يُغْنِي مِنَ اللَّهَبِ (31) إِنَّهَا تَرْمِي بِشَرَرٍ كَالْقَصْرِ (32) كَأَنَّهُ جِمَالَتٌ صُفْرٌ (33) وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ (34) هَٰذَا يَوْمُ لَا يَنطِقُونَ (35) وَلَا يُؤْذَنُ لَهُمْ فَيَعْتَذِرُونَ (36) وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ (37) هَٰذَا يَوْمُ الْفَصْلِ ۖ جَمَعْنَاكُمْ وَالْأَوَّلِينَ (38) فَإِن كَانَ لَكُمْ كَيْدٌ فَكِيدُونِ (39) وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ (40) إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي ظِلَالٍ وَعُيُونٍ (41) وَفَوَاكِهَ مِمَّا يَشْتَهُونَ (42) كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ (43) إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ (44) وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ (45) كُلُوا وَتَمَتَّعُوا قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجْرِمُونَ (46) وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ (47) وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ارْكَعُوا لَا يَرْكَعُونَ (48) وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ (49) فَبِأَيِّ حَدِيثٍ بَعْدَهُ يُؤْمِنُونَ (50)
الصفحة Page 581
(20) Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa?
(21) Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti?
(22) Mpaka muda maalumu?
(23) Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria.
(24) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
(25) Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya
(26) Walio hai na maiti?
(27) Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu?
(28) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
(29) Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha!
(30) Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu!
(31) Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako.
(32) Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba!
(33) Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano!
(34) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
(35) Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu,
(36) Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru.
(37) Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
(38) Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia.
(39) Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi!
(40) Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
(41) Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem,
(42) Na matunda wanayo yapenda,
(43) Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda.
(44) Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema.
(45) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
(46) Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu!
(47) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
(48) Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami.
(49) Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
(50) Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022