(102) Hawatausikia mvumo wake, na wao watadumu katika yale zinayo yatamani nafsi zao.
(103) Hicho Kitisho Kikubwa hakito wahuzunisha. Na Malaika watawapokea (kwa kuwaambia): Hii ndiyo Siku yenu mliyo kuwa mkiahidiwa!
(104) Siku tutakapo zikunja mbingu kama mkunjo wa karatasi za vitabu. Kama tulivyo anza umbo la mwanzo tutalirudisha tena. Ni ahadi iliyo juu yetu. Hakika Sisi ni watendao.
(105) Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema.
(106) Hakika katika haya yapo mawaidha kwa watu wafanyao ibada.
(107) Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.
(108) Sema: Hakika imefunuliwa kwangu ya kwamba hakika Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Je! Mmesilimu?
(109) Na kama wakigeuka, basi sema: Nimekutangazieni sawa sawa, wala sijui yako karibu au mbali hayo mliyo ahidiwa.
(110) Hakika Yeye anajua kauli ya dhaahiri na anajua myafichayo.
(111) Wala sijui pengine huu ni mtihani tu kwenu na starehe mpaka muda kidogo.
(112) Sema: Mola wangu Mlezi! Hukumu kwa haki. Na Mola wetu Mlezi ni Mwingi wa Rehema, aombwaye msaada juu ya mnayo yazua.