المعارج   سورة  : Al-Ma'aarij


سورة Sura   المعارج   Al-Ma'aarij
فَلَيْسَ لَهُ الْيَوْمَ هَاهُنَا حَمِيمٌ (35) وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنْ غِسْلِينٍ (36) لَّا يَأْكُلُهُ إِلَّا الْخَاطِئُونَ (37) فَلَا أُقْسِمُ بِمَا تُبْصِرُونَ (38) وَمَا لَا تُبْصِرُونَ (39) إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ (40) وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَاعِرٍ ۚ قَلِيلًا مَّا تُؤْمِنُونَ (41) وَلَا بِقَوْلِ كَاهِنٍ ۚ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ (42) تَنزِيلٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ (43) وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَيْنَا بَعْضَ الْأَقَاوِيلِ (44) لَأَخَذْنَا مِنْهُ بِالْيَمِينِ (45) ثُمَّ لَقَطَعْنَا مِنْهُ الْوَتِينَ (46) فَمَا مِنكُم مِّنْ أَحَدٍ عَنْهُ حَاجِزِينَ (47) وَإِنَّهُ لَتَذْكِرَةٌ لِّلْمُتَّقِينَ (48) وَإِنَّا لَنَعْلَمُ أَنَّ مِنكُم مُّكَذِّبِينَ (49) وَإِنَّهُ لَحَسْرَةٌ عَلَى الْكَافِرِينَ (50) وَإِنَّهُ لَحَقُّ الْيَقِينِ (51) فَسَبِّحْ بِاسْمِ رَبِّكَ الْعَظِيمِ (52)
المعارج Al-Ma'aarij
سَأَلَ سَائِلٌ بِعَذَابٍ وَاقِعٍ (1) لِّلْكَافِرِينَ لَيْسَ لَهُ دَافِعٌ (2) مِّنَ اللَّهِ ذِي الْمَعَارِجِ (3) تَعْرُجُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ (4) فَاصْبِرْ صَبْرًا جَمِيلًا (5) إِنَّهُمْ يَرَوْنَهُ بَعِيدًا (6) وَنَرَاهُ قَرِيبًا (7) يَوْمَ تَكُونُ السَّمَاءُ كَالْمُهْلِ (8) وَتَكُونُ الْجِبَالُ كَالْعِهْنِ (9) وَلَا يَسْأَلُ حَمِيمٌ حَمِيمًا (10)
الصفحة Page 568
(35) Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu,
(36) Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni.
(37) Chakula hicho hawakili ila wakosefu.
(38) Basi naapa kwa mnavyo viona,
(39) Na msivyo viona,
(40) Kwa hakika hii ni kauli iliyo letwa na Mjumbe mwenye hishima.
(41) Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayo yaamini.
(42) Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo yakumbuka.
(43) Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
(44) Na lau kama angeli tuzulia baadhi ya maneno tu,
(45) Bila ya shaka tungeli mshika kwa mkono wa kulia,
(46) Kisha kwa hakika tungeli mkata mshipa mkubwa wa moyo!
(47) Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeli weza kutuzuia.
(48) Kwa hakika hii ni mawaidha kwa wachamngu.
(49) Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanao kadhibisha.
(50) Na hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa wanao kataa.
(51) Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini.
(52) Basi litakase jina la Mola wako Mlezi Mtukufu.
المعارج Al-Ma'aarij
(1) Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea,
(2) Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia -
(3) Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja.
(4) Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu!
(5) Basi subiri kwa subira njema.
(6) Hakika wao wanaiona iko mbali,
(7) Na Sisi tunaiona iko karibu.
(8) Siku ambayo mbingu zitakapo kuwa kama maadeni iliyo yayushwa.
(9) Na milima itakuwa kama sufi.
(10) Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake.
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022