البينة   سورة  : Al-Bayyina


سورة Sura   البينة   Al-Bayyina
جَزَاؤُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتُ عَدْنٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۖ رَّضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ ذَٰلِكَ لِمَنْ خَشِيَ رَبَّهُ (8)
الزلزلة Az-Zalzala
إِذَا زُلْزِلَتِ الْأَرْضُ زِلْزَالَهَا (1) وَأَخْرَجَتِ الْأَرْضُ أَثْقَالَهَا (2) وَقَالَ الْإِنسَانُ مَا لَهَا (3) يَوْمَئِذٍ تُحَدِّثُ أَخْبَارَهَا (4) بِأَنَّ رَبَّكَ أَوْحَىٰ لَهَا (5) يَوْمَئِذٍ يَصْدُرُ النَّاسُ أَشْتَاتًا لِّيُرَوْا أَعْمَالَهُمْ (6) فَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْرًا يَرَهُ (7) وَمَن يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرًّا يَرَهُ (8)
العاديات Al-Aadiyaat
وَالْعَادِيَاتِ ضَبْحًا (1) فَالْمُورِيَاتِ قَدْحًا (2) فَالْمُغِيرَاتِ صُبْحًا (3) فَأَثَرْنَ بِهِ نَقْعًا (4) فَوَسَطْنَ بِهِ جَمْعًا (5) إِنَّ الْإِنسَانَ لِرَبِّهِ لَكَنُودٌ (6) وَإِنَّهُ عَلَىٰ ذَٰلِكَ لَشَهِيدٌ (7) وَإِنَّهُ لِحُبِّ الْخَيْرِ لَشَدِيدٌ (8) ۞ أَفَلَا يَعْلَمُ إِذَا بُعْثِرَ مَا فِي الْقُبُورِ (9)
الصفحة Page 599
(8) Malipo yao kwa Mola wao Mlezi ni Bustani za daima, zipitazo mito kati yake. Wakae humo milele. Mwenyezi Mungu yu radhi nao, na wao waradhi naye. Hayo ni kwa anaye mwogopa Mola wake Mlezi.
الزلزلة Az-Zalzala
(1) Itakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake!
(2) Na itakapo toa ardhi mizigo yake!
(3) Na mtu akasema: Ina nini?
(4) Siku hiyo itahadithia khabari zake.
(5) Kwa sababu Mola wake Mlezi ameifunulia!
(6) Siku hiyo watu watatoka kwa mfarakano wakaonyweshwe vitendo vyao!
(7) Basi anaye tenda chembe ya wema, atauona!
(8) Na anaye tenda chembe ya uovu atauona!
العاديات Al-Aadiyaat
(1) Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua,
(2) Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini,
(3) Wakishambulia wakati wa asubuhi,
(4) Huku wakitimua vumbi,
(5) Na wakijitoma kati ya kundi,
(6) Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi!
(7) Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo!
(8) Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali!
(9) Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini?
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022