ص Saad
(1) S'ad, Naapa kwa Qur'ani yenye mawaidha.
(2) Lakini walio kufuru wamo katika majivuno na upinzani
(3) Mataifa mangapi tumeyaangamiza kabla yao, na wakapiga kelele, lakini wakati wa kuokoka ulikwisha pita.
(4) Na walistaajabu kuwajia mwonyaji anaye tokana nao wenyewe, na makafiri wakasema: Huyu ni mchawi, mwongo.
(5) Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu.
(6) Na wakaondoka wakubwa wao wakiwaambia: Nendeni zenu na dumuni na miungu yenu, kwani hili ni jambo lililo pangwa.
(7) Sisi hatukusikia haya katika mila hii ya mwisho. Haya si chochote ila ni uzushi tu.
(8) Ati yeye tu ndiye aliye teremshiwa mawaidha peke yake katika sisi? Lakini hao wana shaka na mawaidha yangu, bali hawajaionja adhabu yangu.
(9) Au wanazo wao khazina za rehema za Mola wako Mlezi, Mwenye nguvu, Mpaji?
(10) Au wao wana ufalme wa mbingu na ardhi na viliomo kati yao? Basi nawazipande njia za kwendea huko!
(11) Hao ni askari watao shindwa miongoni mwa makundi yatayo shindwa.
(12) Walikanusha kabla yao kaumu ya Nuhu, na kina A'adi na Firauni mwenye majengo.
(13) Na Thamud na kaumu Lut'i na watu wa Machakani. Hayo ndiyo makundi.
(14) Hao wote waliwakadhibisha Mitume; basi wakastahiki adhabu yangu.
(15) Na hawa hawangojei ila ukelele mmoja tu usio na muda.
(16) Na wao husema: Mola wetu Mlezi! Tuletee upesi sehemu yetu ya adhabu kabla ya Siku ya Hisabu.