(31) AKASEMA: Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mlio tumwa?
(32) Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu,
(33) Tuwatupie mawe ya udongo,
(34) Yaliyo tiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanao pindukia mipaka.
(35) Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walio amini.
(36) Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu!
(37) Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanao iogopa adhabu chungu.
(38) Na katika khabari za Musa, tulipo mtuma kwa Firauni na hoja wazi.
(39) Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake na akasema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu!
(40) Basi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, na yeye ndiye wa kulaumiwa.
(41) Na katika khabari za A'di tulipo wapelekea upepo wa kukata uzazi.
(42) Haukuacha chochote ulicho kifikia ila ulikifanya kama kilio nyambuka.
(43) Na katika khabari za Thamudi walipo ambiwa: Jifurahisheni kwa muda mdogo tu.
(44) Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi uliwanyakua moto wa radi nao wanaona.
(45) Basi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenye kujitetea.
(46) Na kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwa watu wapotovu.
(47) Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio twenye uwezo wa kuzitanua.
(48) Na ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazuri namna gani Sisi!
(49) Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie.
(50) Basi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.
(51) Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.