(32) Au hizo akili zao ndio zinawaamrisha haya, au wao basi ni watu majeuri tu?
(33) Au ndio wanasema: Ameitunga hii! Bali basi tu hawaamini!
(34) Basi nawalete masimulizi kama haya ikiwa wao wanasema kweli.
(35) Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji?
(36) Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana na yakini.
(37) Au wanazo khazina za Mola wako Mlezi au wao ndio wenye madaraka?
(38) Au wanazo ngazi za kusikilizia? Basi huyo msikilizaji wao na alete hoja ilio wazi!
(39) Au Yeye Mwenyezi Mungu ana wasichana, na nyinyi ndio mna wavulana?
(40) Au wewe unawaomba ujira, na kwa hivyo ndio wanaelemewa na uzito wa gharama?
(41) Au wanayo ilimu ya ghaibu, nao wameandika?
(42) Au wanataka kufanya vitimbi tu? Lakini hao walio kufuru ndio watakao tegeka.
(43) Au wanae mungu asiye kuwa Mwenyezi Mungu? Subhanallah! Ametaksika Mwenyezi Mungu na hao wanao washirikisha naye.
(44) Na hata wange ona pande linatoka mbinguni linaanguka wange sema: Ni mawingu yaliyo bebana.
(45) Basi waache mpaka wakutane na siku yao watakapo hilikishwa.
(46) Siku ambayo hila zao hazitawafaa hata kidogo, wala wao hawatanusuriwa.
(47) Na hakika walio dhulumu watapata adhabu nyengine isiyo kuwa hii, lakini wengi wao hawajui.
(48) Na ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi. Kwani wewe hakika uko mbele ya macho yetu, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi unapo simama,
(49) Na usiku pia mtakase, na zinapo kuchwa nyota.