(6) Ni chemchem watakao inywa waja wa Mwenyezi Mungu, wakiifanya imiminike kwa wingi.
(7) Wanatimiza ahadi, na wanaiogopa siku ambayo shari yake inaenea sana,
(8) Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa.
(9) Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani.
(10) Hakika sisi tunaiogopa kwa Mola wetu Mlezi hiyo siku yenye shida na taabu.
(11) Basi Mwenyezi Mungu atawalinda na shari ya siku hiyo, na atawakutanisha na raha na furaha.
(12) Na atawajazi Bustani za Peponi na maguo ya hariri kwa vile walivyo subiri.
(13) Humo wataegemea juu ya viti vya enzi, hawataona humo jua kali wala baridi kali.
(14) Na vivuli vyake vitakuwa karibu yao, na mashada ya matunda yataning'inia mpaka chini.
(15) Na watapitishiwa vyombo vya fedha na vikombe vya vigae,
(16) Vya fedha safi kama kiyoo, wamevipima kwa vipimo.
(17) Na humo watanyweshwa kinywaji kilicho changanyika na tangawizi.
(18) Hiyo ni chemchem iliyo humo inaitwa Salsabil.
(19) Na watawazungukia kuwatumikia wavulana wasio pevuka, ukiwaona utawafikiri ni lulu zilizo tawanywa.
(20) Na utakapo yaona, utakuwa umeona neema na ufalme mkubwa.
(21) Juu yao zipo nguo za hariri laini za kijani kibichi, na hariri nzito ya at'ilasi. Na watavikwa vikuku vya fedha, na Mola wao Mlezi atawanywesha kinywaji safi kabisa.
(22) Hakika haya ni malipo yenu; na juhudi zenu zimekubaliwa.
(23) Hakika Sisi tumekuteremshia Qur'ani kidogo kidogo.
(24) Basi ngojea hukumu ya Mola wako Mlezi wala usimt'ii miongoni mwao mwenye dhambi au mwenye kufuru.
(25) Na likumbuke jina la Mola wako Mlezi asubuhi na jioni;