التكوير   سورة  : At-Takwir


سورة Sura   التكوير   At-Takwir
التكوير At-Takwir
إِذَا الشَّمْسُ كُوِّرَتْ (1) وَإِذَا النُّجُومُ انكَدَرَتْ (2) وَإِذَا الْجِبَالُ سُيِّرَتْ (3) وَإِذَا الْعِشَارُ عُطِّلَتْ (4) وَإِذَا الْوُحُوشُ حُشِرَتْ (5) وَإِذَا الْبِحَارُ سُجِّرَتْ (6) وَإِذَا النُّفُوسُ زُوِّجَتْ (7) وَإِذَا الْمَوْءُودَةُ سُئِلَتْ (8) بِأَيِّ ذَنبٍ قُتِلَتْ (9) وَإِذَا الصُّحُفُ نُشِرَتْ (10) وَإِذَا السَّمَاءُ كُشِطَتْ (11) وَإِذَا الْجَحِيمُ سُعِّرَتْ (12) وَإِذَا الْجَنَّةُ أُزْلِفَتْ (13) عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا أَحْضَرَتْ (14) فَلَا أُقْسِمُ بِالْخُنَّسِ (15) الْجَوَارِ الْكُنَّسِ (16) وَاللَّيْلِ إِذَا عَسْعَسَ (17) وَالصُّبْحِ إِذَا تَنَفَّسَ (18) إِنَّهُ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ (19) ذِي قُوَّةٍ عِندَ ذِي الْعَرْشِ مَكِينٍ (20) مُّطَاعٍ ثَمَّ أَمِينٍ (21) وَمَا صَاحِبُكُم بِمَجْنُونٍ (22) وَلَقَدْ رَآهُ بِالْأُفُقِ الْمُبِينِ (23) وَمَا هُوَ عَلَى الْغَيْبِ بِضَنِينٍ (24) وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَيْطَانٍ رَّجِيمٍ (25) فَأَيْنَ تَذْهَبُونَ (26) إِنْ هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ (27) لِمَن شَاءَ مِنكُمْ أَن يَسْتَقِيمَ (28) وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ (29)
الصفحة Page 586
التكوير At-Takwir
(1) Jua litakapo kunjwa,
(2) Na nyota zikazimwa,
(3) Na milima ikaondolewa,
(4) Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa wasishughulikiwe,
(5) Na wanyama wa mwituni wakakusanywa,
(6) Na bahari zikawaka moto,
(7) Na nafsi zikaunganishwa,
(8) Na msichana aliye zikwa hai atapo ulizwa,
(9) Kwa kosa gani aliuliwa?
(10) Na madaftari yatakapo enezwa,
(11) Na mbingu itapo tanduliwa,
(12) Na Jahannamu itapo chochewa,
(13) Na Pepo ikasogezwa,
(14) Kila nafsi itajua ilicho kihudhurisha.
(15) Naapa kwa nyota zinapo rejea nyuma,
(16) Zinazo kwenda, kisha zikajificha,
(17) Na kwa usiku unapo pungua,
(18) Na kwa asubuhi inapo pambazuka,
(19) Kwamba hakika bila ya shaka hii ni kauli ya Mjumbe mtukufu,
(20) Mwenye nguvu na mwenye cheo kwa huyo Mwenye Kiti cha Enzi,
(21) Anaye t'iiwa, tena muaminifu.
(22) Na wala huyu mwenzenu hana wazimu.
(23) Na hakika yeye alimwona kwenye upeo wa macho ulio safi.
(24) Wala yeye si bakhili kwa mambo ya ghaibu.
(25) Wala hii si kauli ya Shetani maluuni.
(26) Basi mnakwenda wapi?
(27) Haikuwa hii ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.
(28) Kwa yule miongoni mwenu anaye taka kwenda sawa.
(29) Wala nyinyi hamtataka isipo kuwa atake Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022