الغاشية   سورة  : Al-Ghaashiya


سورة Sura   الغاشية   Al-Ghaashiya
بَلْ تُؤْثِرُونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا (16) وَالْآخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ (17) إِنَّ هَٰذَا لَفِي الصُّحُفِ الْأُولَىٰ (18) صُحُفِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ (19)
الغاشية Al-Ghaashiya
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ الْغَاشِيَةِ (1) وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَاشِعَةٌ (2) عَامِلَةٌ نَّاصِبَةٌ (3) تَصْلَىٰ نَارًا حَامِيَةً (4) تُسْقَىٰ مِنْ عَيْنٍ آنِيَةٍ (5) لَّيْسَ لَهُمْ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٍ (6) لَّا يُسْمِنُ وَلَا يُغْنِي مِن جُوعٍ (7) وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاعِمَةٌ (8) لِّسَعْيِهَا رَاضِيَةٌ (9) فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ (10) لَّا تَسْمَعُ فِيهَا لَاغِيَةً (11) فِيهَا عَيْنٌ جَارِيَةٌ (12) فِيهَا سُرُرٌ مَّرْفُوعَةٌ (13) وَأَكْوَابٌ مَّوْضُوعَةٌ (14) وَنَمَارِقُ مَصْفُوفَةٌ (15) وَزَرَابِيُّ مَبْثُوثَةٌ (16) أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ (17) وَإِلَى السَّمَاءِ كَيْفَ رُفِعَتْ (18) وَإِلَى الْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ (19) وَإِلَى الْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ (20) فَذَكِّرْ إِنَّمَا أَنتَ مُذَكِّرٌ (21) لَّسْتَ عَلَيْهِم بِمُصَيْطِرٍ (22) إِلَّا مَن تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ (23) فَيُعَذِّبُهُ اللَّهُ الْعَذَابَ الْأَكْبَرَ (24) إِنَّ إِلَيْنَا إِيَابَهُمْ (25) ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا حِسَابَهُم (26)
الصفحة Page 592
(16) Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia!
(17) Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.
(18) Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo,
(19) Vitabu vya Ibrahimu na Musa.
الغاشية Al-Ghaashiya
(1) Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza?
(2) Siku hiyo nyuso zitainama,
(3) Zikifanya kazi, nazo taabani.
(4) Ziingie katika Moto unao waka -
(5) Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka.
(6) Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba.
(7) Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa.
(8) Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu.
(9) Zitakuwa radhi kwa juhudi yao,
(10) Katika Bustani ya juu.
(11) Hawatasikia humo upuuzi.
(12) Humo imo chemchem inayo miminika.
(13) Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa,
(14) Na bilauri zilizo pangwa,
(15) Na matakia safu safu,
(16) Na mazulia yaliyo tandikwa.
(17) Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa?
(18) Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa?
(19) Na milima jinsi ilivyo thibitishwa?
(20) Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa?
(21) Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji.
(22) Wewe si mwenye kuwatawalia.
(23) Lakini anaye rudi nyuma na kukataa,
(24) Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa!
(25) Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao.
(26) Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao!
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022