الضحى   سورة  : Ad-Dhuhaa


سورة Sura   الضحى   Ad-Dhuhaa
لَا يَصْلَاهَا إِلَّا الْأَشْقَى (15) الَّذِي كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ (16) وَسَيُجَنَّبُهَا الْأَتْقَى (17) الَّذِي يُؤْتِي مَالَهُ يَتَزَكَّىٰ (18) وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُ مِن نِّعْمَةٍ تُجْزَىٰ (19) إِلَّا ابْتِغَاءَ وَجْهِ رَبِّهِ الْأَعْلَىٰ (20) وَلَسَوْفَ يَرْضَىٰ (21)
الضحى Ad-Dhuhaa
وَالضُّحَىٰ (1) وَاللَّيْلِ إِذَا سَجَىٰ (2) مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ (3) وَلَلْآخِرَةُ خَيْرٌ لَّكَ مِنَ الْأُولَىٰ (4) وَلَسَوْفَ يُعْطِيكَ رَبُّكَ فَتَرْضَىٰ (5) أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًا فَآوَىٰ (6) وَوَجَدَكَ ضَالًّا فَهَدَىٰ (7) وَوَجَدَكَ عَائِلًا فَأَغْنَىٰ (8) فَأَمَّا الْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ (9) وَأَمَّا السَّائِلَ فَلَا تَنْهَرْ (10) وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ (11)
الشرح Ash-Sharh
أَلَمْ نَشْرَحْ لَكَ صَدْرَكَ (1) وَوَضَعْنَا عَنكَ وِزْرَكَ (2) الَّذِي أَنقَضَ ظَهْرَكَ (3) وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ (4) فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا (5) إِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا (6) فَإِذَا فَرَغْتَ فَانصَبْ (7) وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَارْغَب (8)
الصفحة Page 596
(15) Hatauingia ila mwovu kabisa!
(16) Anaye kadhibisha na kupa mgongo.
(17) Na mchamngu ataepushwa nao,
(18) Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa.
(19) Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa.
(20) Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa.
(21) Naye atakuja ridhika!
الضحى Ad-Dhuhaa
(1) Naapa kwa mchana!
(2) Na kwa usiku unapo tanda!
(3) Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.
(4) Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia.
(5) Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.
(6) Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi?
(7) Na akakukuta umepotea akakuongoa?
(8) Akakukuta mhitaji akakutosheleza?
(9) Basi yatima usimwonee!
(10) Na anaye omba au kuuliza usimkaripie!
(11) Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie.
الشرح Ash-Sharh
(1) Hatukukunjulia kifua chako?
(2) Na tukakuondolea mzigo wako,
(3) Ulio vunja mgongo wako?
(4) Na tukakunyanyulia utajo wako?
(5) Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi,
(6) Hakika pamoja na uzito upo wepesi.
(7) Na ukipata faragha, fanya juhudi.
(8) Na Mola wako Mlezi ndio mshughulikie.
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022