(64) Au nani anaye uanzisha uumbaji, kisha akaurejesha? Na nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema: Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema kweli.
(65) Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye ya ghaibu isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Wala wao hawajui lini watafufuliwa.
(66) Kwani huo ujuzi wao umefikilia kuijua Akhera? Bali wao wamo katika shaka nayo tu, bali wao ni vipofu nayo.
(67) Na wakasema walio kufuru: Tutapo kuwa mchanga, sisi na baba zetu, hivyo kweli tutakuja tolewa?
(68) Haya haya tuliahidiwa sisi na baba zetu zamani. Hayakuwa haya ila ni hadithi za uwongo za watu wa kale.
(69) Sema: Nendeni katika ardhi, na tazameni ulikuwaje mwisho wa wakosefu.
(70) Wala usiwahuzunukie wala usiwe katika dhiki kwa sababu ya hila zao wanazo zifanya.
(71) Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa mnasema kweli?
(72) Sema: Asaa ni karibu kukufikieni sehemu ya yale mnayo yahimiza.
(73) Na hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye fadhila kwa watu, lakini wengi wao hawashukuru.
(74) Na hakika Mola wako Mlezi anayajua yanayo ficha vifua vyao na wanayo yatangaza.
(75) Na hakuna siri katika mbingu na ardhi ila imo katika Kitabu kinacho bainisha.
(76) Hakika Qur'ani hii inawasimulia Wana wa Israili mengi wanayo khitalifiana nayo.