الدخان   سورة  : Ad-Dukhaan


سورة Sura   الدخان   Ad-Dukhaan
إِنَّ يَوْمَ الْفَصْلِ مِيقَاتُهُمْ أَجْمَعِينَ (40) يَوْمَ لَا يُغْنِي مَوْلًى عَن مَّوْلًى شَيْئًا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ (41) إِلَّا مَن رَّحِمَ اللَّهُ ۚ إِنَّهُ هُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ (42) إِنَّ شَجَرَتَ الزَّقُّومِ (43) طَعَامُ الْأَثِيمِ (44) كَالْمُهْلِ يَغْلِي فِي الْبُطُونِ (45) كَغَلْيِ الْحَمِيمِ (46) خُذُوهُ فَاعْتِلُوهُ إِلَىٰ سَوَاءِ الْجَحِيمِ (47) ثُمَّ صُبُّوا فَوْقَ رَأْسِهِ مِنْ عَذَابِ الْحَمِيمِ (48) ذُقْ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْكَرِيمُ (49) إِنَّ هَٰذَا مَا كُنتُم بِهِ تَمْتَرُونَ (50) إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي مَقَامٍ أَمِينٍ (51) فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ (52) يَلْبَسُونَ مِن سُندُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُّتَقَابِلِينَ (53) كَذَٰلِكَ وَزَوَّجْنَاهُم بِحُورٍ عِينٍ (54) يَدْعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَاكِهَةٍ آمِنِينَ (55) لَا يَذُوقُونَ فِيهَا الْمَوْتَ إِلَّا الْمَوْتَةَ الْأُولَىٰ ۖ وَوَقَاهُمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ (56) فَضْلًا مِّن رَّبِّكَ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ (57) فَإِنَّمَا يَسَّرْنَاهُ بِلِسَانِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ (58) فَارْتَقِبْ إِنَّهُم مُّرْتَقِبُونَ (59)
الصفحة Page 498
(40) Hakika siku ya Uamuzi ni wakati ulio wekwa kwa wao wote.
(41) Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa.
(42) Isipo kuwa atakaye mrehemu Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.
(43) Hakika Mti wa Zaqqum,
(44) Ni chakula cha mwenye dhambi.
(45) Kama shaba iliyo yayushwa, hutokota matumboni
(46) Kama kutokota kwa maji ya moto.
(47) (Itasemwa:) Mkamateni na mtupeni katikati ya Jahannamu!
(48) Kisha mmwagieni juu ya kichwa chake adhabu ya maji yanayo chemka.
(49) Onja! Ati wewe ndiye mwenye nguvu, mtukufu!
(50) Hakika haya ndiyo mliyo kuwa mkiyatilia shaka.
(51) Hakika wachamngu watakuwa katika mahali pa amani,
(52) Katika mabustani na chemchem,
(53) Watavaa hariri nyepesi na hariri nzito wakikabiliana,
(54) Hivi ndivyo itakavyo kuwa, na tutawaoza mahurilaini.
(55) Humo watataka kila aina ya matunda, na wakae kwa amani.
(56) Humo hawataonja mauti ila mauti yale ya kwanza, na (Mwenyezi Mungu) atawalinda na adhabu ya Jahannamu,
(57) Kuwa ni fadhila zitokazo kwa Mola wako Mlezi. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
(58) Basi tumeifanya nyepesi hii Qur'ani kwa ulimi wako, ili wapate kukumbuka.
(59) Ngoja tu, na wao wangoje pia.
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022