الرحمن   سورة  : Ar-Rahmaan


سورة Sura   الرحمن   Ar-Rahmaan
يُعْرَفُ الْمُجْرِمُونَ بِسِيمَاهُمْ فَيُؤْخَذُ بِالنَّوَاصِي وَالْأَقْدَامِ (41) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (42) هَٰذِهِ جَهَنَّمُ الَّتِي يُكَذِّبُ بِهَا الْمُجْرِمُونَ (43) يَطُوفُونَ بَيْنَهَا وَبَيْنَ حَمِيمٍ آنٍ (44) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (45) وَلِمَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ جَنَّتَانِ (46) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (47) ذَوَاتَا أَفْنَانٍ (48) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (49) فِيهِمَا عَيْنَانِ تَجْرِيَانِ (50) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (51) فِيهِمَا مِن كُلِّ فَاكِهَةٍ زَوْجَانِ (52) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (53) مُتَّكِئِينَ عَلَىٰ فُرُشٍ بَطَائِنُهَا مِنْ إِسْتَبْرَقٍ ۚ وَجَنَى الْجَنَّتَيْنِ دَانٍ (54) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (55) فِيهِنَّ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ (56) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (57) كَأَنَّهُنَّ الْيَاقُوتُ وَالْمَرْجَانُ (58) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (59) هَلْ جَزَاءُ الْإِحْسَانِ إِلَّا الْإِحْسَانُ (60) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (61) وَمِن دُونِهِمَا جَنَّتَانِ (62) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (63) مُدْهَامَّتَانِ (64) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (65) فِيهِمَا عَيْنَانِ نَضَّاخَتَانِ (66) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (67)
الصفحة Page 533
(41) Watajuulikana wakosefu kwa alama zao, basi watashikwa kwa nywele zao za utosini na kwa miguu.
(42) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(43) Hii ndiyo Jahannamu ambayo wakosefu wakiikanusha.
(44) Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto yanayo chemka.
(45) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(46) Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi atapata Bustani mbili.
(47) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(48) Bustani zenye matawi yaliyo tanda.
(49) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(50) Ndani yake zimo chemchem mbili zinazo pita.
(51) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(52) Humo katika kila matunda zimo namna mbili.
(53) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(54) Wawe wameegemea matandiko yenye bit'ana ya hariri nzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu.
(55) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(56) Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao; hajawagusa mtu kabla yao wala jini.
(57) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(58) Kama kwamba wao ni yakuti na marijani.
(59) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha.
(60) Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani?
(61) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(62) Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyengine mbili.
(63) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(64) Za kijani kibivu.
(65) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(66) Na chemchem mbili zinazo furika.
(67) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022