الرحمن   سورة  : Ar-Rahmaan


سورة Sura   الرحمن   Ar-Rahmaan
رَبُّ الْمَشْرِقَيْنِ وَرَبُّ الْمَغْرِبَيْنِ (17) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (18) مَرَجَ الْبَحْرَيْنِ يَلْتَقِيَانِ (19) بَيْنَهُمَا بَرْزَخٌ لَّا يَبْغِيَانِ (20) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (21) يَخْرُجُ مِنْهُمَا اللُّؤْلُؤُ وَالْمَرْجَانُ (22) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (23) وَلَهُ الْجَوَارِ الْمُنشَآتُ فِي الْبَحْرِ كَالْأَعْلَامِ (24) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (25) كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ (26) وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ (27) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (28) يَسْأَلُهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ كُلَّ يَوْمٍ هُوَ فِي شَأْنٍ (29) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (30) سَنَفْرُغُ لَكُمْ أَيُّهَ الثَّقَلَانِ (31) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (32) يَا مَعْشَرَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ إِنِ اسْتَطَعْتُمْ أَن تَنفُذُوا مِنْ أَقْطَارِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ فَانفُذُوا ۚ لَا تَنفُذُونَ إِلَّا بِسُلْطَانٍ (33) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (34) يُرْسَلُ عَلَيْكُمَا شُوَاظٌ مِّن نَّارٍ وَنُحَاسٌ فَلَا تَنتَصِرَانِ (35) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (36) فَإِذَا انشَقَّتِ السَّمَاءُ فَكَانَتْ وَرْدَةً كَالدِّهَانِ (37) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (38) فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُسْأَلُ عَن ذَنبِهِ إِنسٌ وَلَا جَانٌّ (39) فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ (40)
الصفحة Page 532
(17) Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili.
(18) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(19) Anaziendesha bahari mbili zikutane;
(20) Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane.
(21) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(22) Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani.
(23) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(24) Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyo undwa kama vilima.
(25) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(26) Kila kilioko juu yake kitatoweka.
(27) Na atabakia Mwenyewe Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.
(28) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(29) Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo.
(30) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(31) Tutakuhisabuni enyi makundi mawili.
(32) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(33) Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka.
(34) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(35) Mtapelekewa muwako wa moto na shaba; wala hamtashinda.
(36) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(37) Itakapo pasuka mbingu ikawa nyekundu kama mafuta.
(38) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
(39) Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini.
(40) Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022