(43) Macho yao yatainama chini, fedheha itawafunika. Na hakika walikuwa wakiitwa wasujudu walipo kuwa wazima -
(44) Basi niache na wanao kadhibisha maneno haya! Tutawavutia kidogo kidogo kwa mahali wasipo pajua.
(45) Na ninawapururia muhula; hakika hila zangu ni imara.
(46) Au unawaomba ujira, na wao wanaemewa na gharama hiyo?
(47) Au iko kwao siri, basi wao wanaiandika?
(48) Basi ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi, wala usiwe kama mmezwa na samaki, alipo nadi naye kazongwa.
(49) Kama isingeli mfikia neema kutoka kwa Mola wake Mlezi, bila ya shaka angeli tupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa.
(50) Lakini Mola wake Mlezi alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema.
(51) Na walio kufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanapo sikia mawaidha, na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu.
(52) Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote.
الحاقة Al-Haaqqa
(1) Tukio la haki.
(2) Nini hilo Tukio la haki?
(3) Na nini kitakujuulisha nini hilo Tukio la haki?
(4) Thamudi na A'di waliukadhibisha Msiba unao situsha.
(5) Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno.
(6) Na ama A'di waliangamizwa kwa upepo mkali usio zuilika.
(7) Alio wapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo bila ya kusita. Utaona watu wamepinduka kama kwamba ni magongo ya mitende yalio wazi ndani.
(8) Basi je! Unamwona mmoja wao aliye baki?