عبس   سورة  : Abasa


سورة Sura   عبس   Abasa
عبس Abasa
عَبَسَ وَتَوَلَّىٰ (1) أَن جَاءَهُ الْأَعْمَىٰ (2) وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُ يَزَّكَّىٰ (3) أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ الذِّكْرَىٰ (4) أَمَّا مَنِ اسْتَغْنَىٰ (5) فَأَنتَ لَهُ تَصَدَّىٰ (6) وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ (7) وَأَمَّا مَن جَاءَكَ يَسْعَىٰ (8) وَهُوَ يَخْشَىٰ (9) فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّىٰ (10) كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ (11) فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ (12) فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ (13) مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍ (14) بِأَيْدِي سَفَرَةٍ (15) كِرَامٍ بَرَرَةٍ (16) قُتِلَ الْإِنسَانُ مَا أَكْفَرَهُ (17) مِنْ أَيِّ شَيْءٍ خَلَقَهُ (18) مِن نُّطْفَةٍ خَلَقَهُ فَقَدَّرَهُ (19) ثُمَّ السَّبِيلَ يَسَّرَهُ (20) ثُمَّ أَمَاتَهُ فَأَقْبَرَهُ (21) ثُمَّ إِذَا شَاءَ أَنشَرَهُ (22) كَلَّا لَمَّا يَقْضِ مَا أَمَرَهُ (23) فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ إِلَىٰ طَعَامِهِ (24) أَنَّا صَبَبْنَا الْمَاءَ صَبًّا (25) ثُمَّ شَقَقْنَا الْأَرْضَ شَقًّا (26) فَأَنبَتْنَا فِيهَا حَبًّا (27) وَعِنَبًا وَقَضْبًا (28) وَزَيْتُونًا وَنَخْلًا (29) وَحَدَائِقَ غُلْبًا (30) وَفَاكِهَةً وَأَبًّا (31) مَّتَاعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَامِكُمْ (32) فَإِذَا جَاءَتِ الصَّاخَّةُ (33) يَوْمَ يَفِرُّ الْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ (34) وَأُمِّهِ وَأَبِيهِ (35) وَصَاحِبَتِهِ وَبَنِيهِ (36) لِكُلِّ امْرِئٍ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ (37) وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُّسْفِرَةٌ (38) ضَاحِكَةٌ مُّسْتَبْشِرَةٌ (39) وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌ (40) تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ (41) أُولَٰئِكَ هُمُ الْكَفَرَةُ الْفَجَرَةُ (42)
الصفحة Page 585
عبس Abasa
(1) Alikunja kipaji na akageuka,
(2) Kwa sababu alimjia kipofu!
(3) Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika?
(4) Au atawaidhika, na mawaidha yamfae?
(5) Ama ajionaye hana haja,
(6) Wewe ndio unamshughulikia?
(7) Na si juu yako kama hakutakasika.
(8) Ama anaye kujia kwa juhudi,
(9) Naye anaogopa,
(10) Ndio wewe unampuuza?
(11) Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana.
(12) Basi anaye penda akumbuke.
(13) Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa,
(14) Zilizo inuliwa, zilizo takaswa.
(15) Zimo mikononi mwa Malaika waandishi,
(16) Watukufu, wema.
(17) Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha?
(18) Kwa kitu gani amemuumba?
(19) Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria.
(20) Kisha akamsahilishia njia.
(21) Kisha akamfisha, akamtia kaburini.
(22) Kisha apendapo atamfufua.
(23) La! Hajamaliza aliyo muamuru.
(24) Hebu mtu na atazame chakula chake.
(25) Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu,
(26) Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu,
(27) Kisha tukaotesha humo nafaka,
(28) Na zabibu, na mimea ya majani,
(29) Na mizaituni, na mitende,
(30) Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara,
(31) Na matunda, na malisho ya wanyama;
(32) Kwa manufaa yenu na mifugo yenu.
(33) Basi utakapo kuja ukelele,
(34) Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye,
(35) Na mamaye na babaye,
(36) Na mkewe na wanawe -
(37) Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha.
(38) Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri,
(39) Zitacheka, zitachangamka;
(40) Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi,
(41) Giza totoro litazifunika,
(42) Hao ndio makafiri watenda maovu.
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022