الشعراء   سورة  : Ash-Shu'araa


سورة Sura   الشعراء   Ash-Shu'araa
مَا أَغْنَىٰ عَنْهُم مَّا كَانُوا يُمَتَّعُونَ (207) وَمَا أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ إِلَّا لَهَا مُنذِرُونَ (208) ذِكْرَىٰ وَمَا كُنَّا ظَالِمِينَ (209) وَمَا تَنَزَّلَتْ بِهِ الشَّيَاطِينُ (210) وَمَا يَنبَغِي لَهُمْ وَمَا يَسْتَطِيعُونَ (211) إِنَّهُمْ عَنِ السَّمْعِ لَمَعْزُولُونَ (212) فَلَا تَدْعُ مَعَ اللَّهِ إِلَٰهًا آخَرَ فَتَكُونَ مِنَ الْمُعَذَّبِينَ (213) وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ (214) وَاخْفِضْ جَنَاحَكَ لِمَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ (215) فَإِنْ عَصَوْكَ فَقُلْ إِنِّي بَرِيءٌ مِّمَّا تَعْمَلُونَ (216) وَتَوَكَّلْ عَلَى الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ (217) الَّذِي يَرَاكَ حِينَ تَقُومُ (218) وَتَقَلُّبَكَ فِي السَّاجِدِينَ (219) إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ (220) هَلْ أُنَبِّئُكُمْ عَلَىٰ مَن تَنَزَّلُ الشَّيَاطِينُ (221) تَنَزَّلُ عَلَىٰ كُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ (222) يُلْقُونَ السَّمْعَ وَأَكْثَرُهُمْ كَاذِبُونَ (223) وَالشُّعَرَاءُ يَتَّبِعُهُمُ الْغَاوُونَ (224) أَلَمْ تَرَ أَنَّهُمْ فِي كُلِّ وَادٍ يَهِيمُونَ (225) وَأَنَّهُمْ يَقُولُونَ مَا لَا يَفْعَلُونَ (226) إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَذَكَرُوا اللَّهَ كَثِيرًا وَانتَصَرُوا مِن بَعْدِ مَا ظُلِمُوا ۗ وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُونَ (227)
الصفحة Page 376
(207) Yatawafaa nini yale waliyo stareheshewa?
(208) Wala hatukuangamiza mji wo wote ila ulikuwa na waonyaji -
(209) Kuwa ni ukumbusho. Wala Sisi hatukuwa wenye kudhulumu.
(210) Wala Mashet'ani hawakuteremka nayo,
(211) Wala haitakiwi kwao, na wala hawawezi.
(212) Hakika hao wametengwa na kusikia.
(213) Basi usimwombe mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu ukawa miongoni mwa watakao adhibiwa.
(214) Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe.
(215) Na watwae kwa upole wanao kufuata miongoni mwa Waumini.
(216) Na ikiwa watakuasi basi sema: Mimi najitenga mbali na hayo mnayo yatenda.
(217) Na umtegemee Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
(218) Ambaye anakuona unapo simama,
(219) Na mageuko yako kati ya wanao sujudu.
(220) Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua.
(221) Je! Nikwambieni nani wanawashukia Mashet'ani?
(222) Wanamshukia kila mzushi mkubwa mwingi wa dhambi.
(223) Wanawapelekea yale wanayo yasikia; na wengi wao ni waongo.
(224) Na watungaji mashairi ni wapotofu ndio wanawafuata.
(225) Je! Huwaoni kwamba wao wanatangatanga katika kila bonde?
(226) Na kwamba wao husema wasiyo yatenda?
(227) Isipo kuwa wale walio amini, na wakatenda mema, na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na wakajitetea wanapo dhulumiwa. Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022