الشعراء   سورة  : Ash-Shu'araa


سورة Sura   الشعراء   Ash-Shu'araa
قَالَ وَمَا عِلْمِي بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ (112) إِنْ حِسَابُهُمْ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّي ۖ لَوْ تَشْعُرُونَ (113) وَمَا أَنَا بِطَارِدِ الْمُؤْمِنِينَ (114) إِنْ أَنَا إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ (115) قَالُوا لَئِن لَّمْ تَنتَهِ يَا نُوحُ لَتَكُونَنَّ مِنَ الْمَرْجُومِينَ (116) قَالَ رَبِّ إِنَّ قَوْمِي كَذَّبُونِ (117) فَافْتَحْ بَيْنِي وَبَيْنَهُمْ فَتْحًا وَنَجِّنِي وَمَن مَّعِيَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ (118) فَأَنجَيْنَاهُ وَمَن مَّعَهُ فِي الْفُلْكِ الْمَشْحُونِ (119) ثُمَّ أَغْرَقْنَا بَعْدُ الْبَاقِينَ (120) إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ (121) وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ (122) كَذَّبَتْ عَادٌ الْمُرْسَلِينَ (123) إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ هُودٌ أَلَا تَتَّقُونَ (124) إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ (125) فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُونِ (126) وَمَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ الْعَالَمِينَ (127) أَتَبْنُونَ بِكُلِّ رِيعٍ آيَةً تَعْبَثُونَ (128) وَتَتَّخِذُونَ مَصَانِعَ لَعَلَّكُمْ تَخْلُدُونَ (129) وَإِذَا بَطَشْتُم بَطَشْتُمْ جَبَّارِينَ (130) فَاتَّقُوا اللَّهَ وَأَطِيعُونِ (131) وَاتَّقُوا الَّذِي أَمَدَّكُم بِمَا تَعْلَمُونَ (132) أَمَدَّكُم بِأَنْعَامٍ وَبَنِينَ (133) وَجَنَّاتٍ وَعُيُونٍ (134) إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ (135) قَالُوا سَوَاءٌ عَلَيْنَا أَوَعَظْتَ أَمْ لَمْ تَكُن مِّنَ الْوَاعِظِينَ (136)
الصفحة Page 372
(112) Akasema: Nayajuaje waliyo kuwa wakiyafanya?
(113) Hisabu yao haiko ila kwa Mola wao Mlezi, laiti mngeli tambua!
(114) Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini.
(115) Mimi si cho chote ila ni Mwonyaji wa dhaahiri shaahiri.
(116) Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe.
(117) Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha.
(118) Basi hukumu baina yangu na wao kwa hukumu yako, na uniokoe mimi na walio pamoja nami, Waumini.
(119) Kwa hivyo tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye katika marikebu iliyo sheheni.
(120) Kisha tukawazamisha baadaye walio bakia.
(121) Hakika katika haya ipo Ishara, lakini si wengi wao walio kuwa Waumini.
(122) Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
(123) Kina A'd waliwakanusha Mitume.
(124) Alipo waambia ndugu yao, Hud: Je! Hamchimngu?
(125) Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
(126) Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
(127) Wala sikutakeni juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
(128) Je! Mnajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho la kufanyia upuuzi?
(129) Na mnajenga majengo ya fakhari kama kwamba mtaishi milele!
(130) Na mnapo tumia nguvu mnatumia nguvu kwa ujabari.
(131) Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini.
(132) Na mcheni aliye kupeni haya mnayo yajua.
(133) Amekupeni wanyama wa kufuga na wana.
(134) Na mabustani na chemchem.
(135) Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku Kubwa.
(136) Wakasema: Ni mamoja kwetu, ukitupa mawaidha au hukuwa miongoni mwa watoao mawaidha.
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022