الشعراء   سورة  : Ash-Shu'araa


سورة Sura   الشعراء   Ash-Shu'araa
فَلَمَّا تَرَاءَى الْجَمْعَانِ قَالَ أَصْحَابُ مُوسَىٰ إِنَّا لَمُدْرَكُونَ (61) قَالَ كَلَّا ۖ إِنَّ مَعِيَ رَبِّي سَيَهْدِينِ (62) فَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنِ اضْرِب بِّعَصَاكَ الْبَحْرَ ۖ فَانفَلَقَ فَكَانَ كُلُّ فِرْقٍ كَالطَّوْدِ الْعَظِيمِ (63) وَأَزْلَفْنَا ثَمَّ الْآخَرِينَ (64) وَأَنجَيْنَا مُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُ أَجْمَعِينَ (65) ثُمَّ أَغْرَقْنَا الْآخَرِينَ (66) إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ (67) وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ (68) وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ إِبْرَاهِيمَ (69) إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ مَا تَعْبُدُونَ (70) قَالُوا نَعْبُدُ أَصْنَامًا فَنَظَلُّ لَهَا عَاكِفِينَ (71) قَالَ هَلْ يَسْمَعُونَكُمْ إِذْ تَدْعُونَ (72) أَوْ يَنفَعُونَكُمْ أَوْ يَضُرُّونَ (73) قَالُوا بَلْ وَجَدْنَا آبَاءَنَا كَذَٰلِكَ يَفْعَلُونَ (74) قَالَ أَفَرَأَيْتُم مَّا كُنتُمْ تَعْبُدُونَ (75) أَنتُمْ وَآبَاؤُكُمُ الْأَقْدَمُونَ (76) فَإِنَّهُمْ عَدُوٌّ لِّي إِلَّا رَبَّ الْعَالَمِينَ (77) الَّذِي خَلَقَنِي فَهُوَ يَهْدِينِ (78) وَالَّذِي هُوَ يُطْعِمُنِي وَيَسْقِينِ (79) وَإِذَا مَرِضْتُ فَهُوَ يَشْفِينِ (80) وَالَّذِي يُمِيتُنِي ثُمَّ يُحْيِينِ (81) وَالَّذِي أَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لِي خَطِيئَتِي يَوْمَ الدِّينِ (82) رَبِّ هَبْ لِي حُكْمًا وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ (83)
الصفحة Page 370
(61) Na yalipo onana majeshi mawili haya, watu wa Musa wakasema: Hakika sisi bila ya shaka tumepatikana!
(62) (Musa) akasema: Hasha! Hakika yu pamoja nami Mola wangu Mlezi. Yeye ataniongoa!
(63) Tulimletea wahyi Musa tukamwambia: Piga bahari kwa fimbo yako. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mlima mkubwa.
(64) Na tukawajongeza hapo wale wengine.
(65) Tukawaokoa Musa na walio kuwa pamoja naye wote.
(66) Kisha tukawazamisha hao wengine.
(67) Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara; lakini wengi wao si katika wenye kuamini.
(68) Na kwa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
(69) Na wasomee khabari za Ibrahim.
(70) Alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Mnaabudu nini?
(71) Wakasema: Tunaabudu masanamu, daima tunayanyenyekea.
(72) Akasema: Je! Yanakusikieni mnapo yaita?
(73) Au yanakufaeni, au yanakudhuruni?
(74) Wakasema: Bali tumewakuta baba zetu wakifanya hivyo hivyo.
(75) Je! Mmewaona hawa mnao waabudu-
(76) Nyinyi na baba zenu wa zamani?
(77) Kwani hakika hao ni adui zangu, isipo kuwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
(78) Ambaye ndiye aliye niumba, na Yeye ndiye ananiongoa,
(79) Na ambaye ndiye ananilisha na kuninywesha.
(80) Na ninapo ugua ni Yeye ndiye anaye niponesha.
(81) Na ambaye atanifisha, na kisha atanihuisha.
(82) Na ambaye ndiye ninaye mtumai kunisamehe makosa yangu Siku ya Malipo.
(83) Mola wangu Mlezi! Nitunukie hukumu na uniunganishe na watendao mema.
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022