الصافات   سورة  : As-Saaffaat


سورة Sura   الصافات   As-Saaffaat
فَكَذَّبُوهُ فَإِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ (127) إِلَّا عِبَادَ اللَّهِ الْمُخْلَصِينَ (128) وَتَرَكْنَا عَلَيْهِ فِي الْآخِرِينَ (129) سَلَامٌ عَلَىٰ إِلْ يَاسِينَ (130) إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ (131) إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُؤْمِنِينَ (132) وَإِنَّ لُوطًا لَّمِنَ الْمُرْسَلِينَ (133) إِذْ نَجَّيْنَاهُ وَأَهْلَهُ أَجْمَعِينَ (134) إِلَّا عَجُوزًا فِي الْغَابِرِينَ (135) ثُمَّ دَمَّرْنَا الْآخَرِينَ (136) وَإِنَّكُمْ لَتَمُرُّونَ عَلَيْهِم مُّصْبِحِينَ (137) وَبِاللَّيْلِ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ (138) وَإِنَّ يُونُسَ لَمِنَ الْمُرْسَلِينَ (139) إِذْ أَبَقَ إِلَى الْفُلْكِ الْمَشْحُونِ (140) فَسَاهَمَ فَكَانَ مِنَ الْمُدْحَضِينَ (141) فَالْتَقَمَهُ الْحُوتُ وَهُوَ مُلِيمٌ (142) فَلَوْلَا أَنَّهُ كَانَ مِنَ الْمُسَبِّحِينَ (143) لَلَبِثَ فِي بَطْنِهِ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ (144) ۞ فَنَبَذْنَاهُ بِالْعَرَاءِ وَهُوَ سَقِيمٌ (145) وَأَنبَتْنَا عَلَيْهِ شَجَرَةً مِّن يَقْطِينٍ (146) وَأَرْسَلْنَاهُ إِلَىٰ مِائَةِ أَلْفٍ أَوْ يَزِيدُونَ (147) فَآمَنُوا فَمَتَّعْنَاهُمْ إِلَىٰ حِينٍ (148) فَاسْتَفْتِهِمْ أَلِرَبِّكَ الْبَنَاتُ وَلَهُمُ الْبَنُونَ (149) أَمْ خَلَقْنَا الْمَلَائِكَةَ إِنَاثًا وَهُمْ شَاهِدُونَ (150) أَلَا إِنَّهُم مِّنْ إِفْكِهِمْ لَيَقُولُونَ (151) وَلَدَ اللَّهُ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ (152) أَصْطَفَى الْبَنَاتِ عَلَى الْبَنِينَ (153)
الصفحة Page 451
(127) Wakamkadhibisha. Basi kwa hakika watahudhurishwa;
(128) Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa.
(129) Na tumemwachia (sifa nzuri) kwa walio kuja baadaye.
(130) Iwe salama kwa Ilyas.
(131) Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema.
(132) Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini.
(133) Na hakika Lut'i bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume.
(134) Tulipo mwokoa yeye na ahali zake wote,
(135) Isipo kuwa mwanamke mkongwe katika wale walio bakia nyuma.
(136) Kisha tukawaangamiza wale wengineo.
(137) Na hakika nyinyi mnawapitia wakati wa asubuhi,
(138) Na usiku. Basi je! Hamyatii akilini?
(139) Na hakika Yunus alikuwa miongoni mwa Mitume.
(140) Alipo kimbia katika jahazi lilio sheheni.
(141) Akaingia katika kupigiwa kura, na akawa katika walio shindwa.
(142) Samaki akammeza hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa.
(143) Na ingeli kuwa hakuwa katika wanao mtakasa Mwenyezi Mungu,
(144) Bila ya shaka angeli kaa ndani yake mpaka siku ya kufufuliwa.
(145) Lakini tulimtupa ufukweni patupu, hali yu mgonjwa.
(146) Na tukauotesha juu yake mmea wa kabila ya mung'unye.
(147) Na tulimtuma kwa watu laki moja au zaidi.
(148) Basi wakaamini, na tukawastarehesha kwa muda.
(149) Basi waulize: Ati Mola wako Mlezi ndiye mwenye watoto wa kike, na wao wanao watoto wa kiume?
(150) Au tumewaumba Malaika kuwa ni wanawake, na wao wakashuhudia?
(151) Ati ni kwa uzushi wao ndio wanasema:
(152) Mwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni waongo!
(153) Ati amekhiari watoto wa kike kuliko wanaume?
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022