الصافات   سورة  : As-Saaffaat


سورة Sura   الصافات   As-Saaffaat
مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ (154) أَفَلَا تَذَكَّرُونَ (155) أَمْ لَكُمْ سُلْطَانٌ مُّبِينٌ (156) فَأْتُوا بِكِتَابِكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ (157) وَجَعَلُوا بَيْنَهُ وَبَيْنَ الْجِنَّةِ نَسَبًا ۚ وَلَقَدْ عَلِمَتِ الْجِنَّةُ إِنَّهُمْ لَمُحْضَرُونَ (158) سُبْحَانَ اللَّهِ عَمَّا يَصِفُونَ (159) إِلَّا عِبَادَ اللَّهِ الْمُخْلَصِينَ (160) فَإِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ (161) مَا أَنتُمْ عَلَيْهِ بِفَاتِنِينَ (162) إِلَّا مَنْ هُوَ صَالِ الْجَحِيمِ (163) وَمَا مِنَّا إِلَّا لَهُ مَقَامٌ مَّعْلُومٌ (164) وَإِنَّا لَنَحْنُ الصَّافُّونَ (165) وَإِنَّا لَنَحْنُ الْمُسَبِّحُونَ (166) وَإِن كَانُوا لَيَقُولُونَ (167) لَوْ أَنَّ عِندَنَا ذِكْرًا مِّنَ الْأَوَّلِينَ (168) لَكُنَّا عِبَادَ اللَّهِ الْمُخْلَصِينَ (169) فَكَفَرُوا بِهِ ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ (170) وَلَقَدْ سَبَقَتْ كَلِمَتُنَا لِعِبَادِنَا الْمُرْسَلِينَ (171) إِنَّهُمْ لَهُمُ الْمَنصُورُونَ (172) وَإِنَّ جُندَنَا لَهُمُ الْغَالِبُونَ (173) فَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ (174) وَأَبْصِرْهُمْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ (175) أَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ (176) فَإِذَا نَزَلَ بِسَاحَتِهِمْ فَسَاءَ صَبَاحُ الْمُنذَرِينَ (177) وَتَوَلَّ عَنْهُمْ حَتَّىٰ حِينٍ (178) وَأَبْصِرْ فَسَوْفَ يُبْصِرُونَ (179) سُبْحَانَ رَبِّكَ رَبِّ الْعِزَّةِ عَمَّا يَصِفُونَ (180) وَسَلَامٌ عَلَى الْمُرْسَلِينَ (181) وَالْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ (182)
الصفحة Page 452
(154) Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi?
(155) Hamkumbuki?
(156) Au mnayo hoja iliyo wazi?
(157) Basi leteni Kitabu chenu kama mnasema kweli.
(158) Na wameweka makhusiano ya nasaba baina yake na majini; na majini wamekwisha jua bila ya shaka kuwa wao watahudhurishwa.
(159) Subhana 'Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo msingizia.
(160) Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa.
(161) Basi hakika nyinyi na mnao waabudu
(162) Hamwezi kuwapoteza
(163) Isipo kuwa yule atakaye ingia Motoni.
(164) Na hapana katika sisi ila anapo mahali pake maalumu.
(165) Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu.
(166) Na hakika sisi ndio wenye kusabihi kutakasa.
(167) Na walikuwapo walio kuwa wakisema:
(168) Tungeli kuwa na Ukumbusho kama wa watu wa zamani,
(169) Bila ya shaka tungeli kuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu wenye ikhlasi.
(170) Lakini waliukataa. Basi watakuja jua.
(171) Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa waja wetu walio tumwa.
(172) Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakao nusuriwa.
(173) Na kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda.
(174) Basi waachilie mbali kwa muda.
(175) Na watazame, nao wataona.
(176) Je! Wanaihimiza adhabu yetu?
(177) Basi itakapo shuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi mbaya kwa walio onywa.
(178) Na waache kwa muda.
(179) Na tazama, na wao wataona.
(180) Subhana Rabbi'l'Izzat Ametakasika Mola Mlezi Mwenye enzi na yale wanayo mzulia.
(181) Na Salamu juu ya Mitume.
(182) Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022