الصافات   سورة  : As-Saaffaat


سورة Sura   الصافات   As-Saaffaat
مَا لَكُمْ لَا تَنَاصَرُونَ (25) بَلْ هُمُ الْيَوْمَ مُسْتَسْلِمُونَ (26) وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ (27) قَالُوا إِنَّكُمْ كُنتُمْ تَأْتُونَنَا عَنِ الْيَمِينِ (28) قَالُوا بَل لَّمْ تَكُونُوا مُؤْمِنِينَ (29) وَمَا كَانَ لَنَا عَلَيْكُم مِّن سُلْطَانٍ ۖ بَلْ كُنتُمْ قَوْمًا طَاغِينَ (30) فَحَقَّ عَلَيْنَا قَوْلُ رَبِّنَا ۖ إِنَّا لَذَائِقُونَ (31) فَأَغْوَيْنَاكُمْ إِنَّا كُنَّا غَاوِينَ (32) فَإِنَّهُمْ يَوْمَئِذٍ فِي الْعَذَابِ مُشْتَرِكُونَ (33) إِنَّا كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِالْمُجْرِمِينَ (34) إِنَّهُمْ كَانُوا إِذَا قِيلَ لَهُمْ لَا إِلَٰهَ إِلَّا اللَّهُ يَسْتَكْبِرُونَ (35) وَيَقُولُونَ أَئِنَّا لَتَارِكُو آلِهَتِنَا لِشَاعِرٍ مَّجْنُونٍ (36) بَلْ جَاءَ بِالْحَقِّ وَصَدَّقَ الْمُرْسَلِينَ (37) إِنَّكُمْ لَذَائِقُو الْعَذَابِ الْأَلِيمِ (38) وَمَا تُجْزَوْنَ إِلَّا مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ (39) إِلَّا عِبَادَ اللَّهِ الْمُخْلَصِينَ (40) أُولَٰئِكَ لَهُمْ رِزْقٌ مَّعْلُومٌ (41) فَوَاكِهُ ۖ وَهُم مُّكْرَمُونَ (42) فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ (43) عَلَىٰ سُرُرٍ مُّتَقَابِلِينَ (44) يُطَافُ عَلَيْهِم بِكَأْسٍ مِّن مَّعِينٍ (45) بَيْضَاءَ لَذَّةٍ لِّلشَّارِبِينَ (46) لَا فِيهَا غَوْلٌ وَلَا هُمْ عَنْهَا يُنزَفُونَ (47) وَعِندَهُمْ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ عِينٌ (48) كَأَنَّهُنَّ بَيْضٌ مَّكْنُونٌ (49) فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَاءَلُونَ (50) قَالَ قَائِلٌ مِّنْهُمْ إِنِّي كَانَ لِي قَرِينٌ (51)
الصفحة Page 447
(25) Mna nini? Mbona hamsaidiani?
(26) Bali hii leo, watasalimu amri.
(27) Watakabiliana wao kwa wao kuulizana.
(28) Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia.
(29) Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini.
(30) Sisi hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu.
(31) Basi hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja tu adhabu.
(32) Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu.
(33) Basi wao kwa hakika siku hiyo watashirikiana katika adhabu pamoja.
(34) Hivyo ndivyo tutakavyo wafanyia wakosefu.
(35) Wao walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu, wakijivuna.
(36) Na wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mtunga mashairi mwendawazimu?
(37) Bali huyu amekuja kwa Haki, na amewasadikisha Mitume.
(38) Hakika nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu.
(39) Wala hamlipwi ila hayo mliyo kuwa mkiyafanya.
(40) Isipo kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa.
(41) Hao ndio watakao pata riziki maalumu,
(42) Matunda, nao watahishimiwa.
(43) Katika Bustani za neema.
(44) Wako juu ya viti wamekabiliana.
(45) Wanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchem
(46) Kinywaji cheupe, kitamu kwa wanywao.
(47) Hakina madhara, wala hakiwaleweshi.
(48) Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha mazuri.
(49) Hao wanawake kama mayai yaliyo hifadhika.
(50) Waingie kuulizana wenyewe kwa wenyewe.
(51) Aseme msemaji mmoja miongoni mwao: Hakika mimi nalikuwa na rafiki
 


اتصل بنا | الملكية الفكرية DCMA | سياسة الخصوصية | Privacy Policy | قيوم المستخدم

آيــــات - القرآن الكريم


© 2022