(103) Basi wote wawili walipo jisalimisha, na akamlaza juu ya kipaji.
(104) Tulimwita: Ewe Ibrahim!
(105) Umekwisha itimiliza ndoto. Hakika hivi ndivyo tunavyo walipa wanao tenda mema.
(106) Hakika haya ni majaribio yaliyo dhaahiri.
(107) Basi tukamtolea fidia kwa dhabihu mtukufu.
(108) Na tukamwachia (sifa njema) kwa watu walio kuja baadaye.
(109) Iwe salama kwa Ibrahim!
(110) Hivi ndivyo tunavyo walipa wanao fanya mema.
(111) Hakika yeye ni katika waja wetu walio amini.
(112) Na tukambashiria kuzaliwa Is-haqa, naye ni Nabii miongoni mwa watu wema.
(113) Na tukambarikia yeye na Is-haqa. Na miongoni mwa dhuriya zao walitokea wema na wenye kudhulumu nafsi zao waziwazi.
(114) Na kwa hakika tuliwafanyia hisani Musa na Haruni.
(115) Na tukawaokoa wao na watu wao kutokana na dhiki kubwa.
(116) Na tukawanusuru; na wakawa wao ndio wenye kushinda.
(117) Na tukawapa wawili hao Kitabu kinacho bainisha.
(118) Na tukawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka.
(119) Na tukawaachia (sifa njema) katika watu walio kuja baadaye.
(120) Iwe salama kwa Musa na Haruni!
(121) Hakika hivyo ndivyo tunavyo walipa walio wema.
(122) Hakika wawili hao ni katika waja wetu walio amini.
(123) Na hakika Ilyas bila ya shaka alikuwa miongoni mwa Mitume.
(124) Alipo waambia watu wake: Hamwogopi?
(125) Mnamwomba Baa'li na mnamwacha Mbora wa waumbaji,
(126) Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu na Mola Mlezi wa baba zenu wa zamani?