(105) Inafaa nisiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila lilio la Haki. Nami hakika nimekujieni na dalili waziwazi kutokana na Mola Mlezi wenu. Basi waache Wana wa Israili wende nami.
(106) Akasema Firauni: Ikiwa umekuja na Ishara, basi ilete ukiwa ni katika wasemao kweli.
(107) Basi akaitupa fimbo yake, na mara ikawa nyoka dhaahiri.
(108) Na akatoa mkono wake, mara ukawa mweupe kwa watazamao.
(109) Wakasema waheshimiwa wa kaumu ya Firauni: Hakika huyo ni mchawi mjuzi.
(110) Anataka kukutoeni katika nchi yenu. Basi mnatoa shauri gani?
(111) Wakasema: Mwache kidogo yeye na nduguye, na watume mijini wakusanyao,
(112) Wakuletee kila mchawi mjuzi.
(113) Wakaja wachawi kwa Firauni, wakasema: Hakika tutapata ujira ikiwa tutashinda.
(114) Akasema: Naam! Nanyi bila ya shaka mtakuwa katika wa karibu nami.
(115) Wakasema: Ewe Musa! Je, utatupa wewe, au tutakuwa sisi tutao tupa?
(116) Akasema: Tupeni! Basi walipo tupa waliyazuga macho ya watu na wakawatia khofu, na wakaleta uchawi mkubwa.
(117) Nasi tukamfunulia Musa kumwambia: Tupa fimbo yako. Mara ikavimeza vyote vile walivyo vibuni.
(118) Kweli ikathibiti na yakabat'ilika waliyo kuwa wakiyatenda.
(119) Kwa hivyo walishindwa hapo, na wakageuka kuwa wadogo.
(120) Na wachawi wakapoomoka wakisujudu.