البقرة Al-Baqara
(1) Alif Lam Mim.
(2) Hiki ni Kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uwongofu kwa wachamungu,
(3) Ambao huyaamini ya ghaibu na hushika Sala, na hutoa katika tuliyo wapa.
(4) Na ambao wanayaamini yaliyo teremshwa kwako, na yaliyo teremshwa kabla yako; na Akhera wana yakini nayo.
(5) Hao wapo juu ya uwongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio walio fanikiwa.